LOGO

 Gyan grabs late winner for Ghana
BAO la dakika ya 92 toka kwa Nahodha Asamoah Gyan limewapa Ghana ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Algeria Mechi ya Kundi C la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, huko Estadio de Mongomo Mjini Mongomo Nchini Equatorial Guinea.
Bao hilo la Gyan lilifungwa Dakika ya 92 na kuweka hai matumaini ya Ghana kutinga Robo Fainali baada ya kufungwa Mechi yao ya kwanza 2-1 na Senegal.
Gyan, ambae hakucheza Mechi na Senegal baada ya kuugua, alifunga Bao hilo katika Dakika 3 za Nyongeza baada ya Dakika 90 kwisha baada ya kupokea Pasi ndefu na kumzidi maarifa Medjani na kisha kuachia Shuti.
Baadae Leo, Senegal na South Africa watacheza Mechi nyingine ya Kundi C.

VIKOSI:
Algeria (4-3-3): M’Bolhi; Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam; Bentaleb, Lacen, Taider; Feghouli, Belfodil, Brahimi.
Ghana (4-4-2): Razak; Afful, Amartey, Mensah, Rahman; Atsu, Acquah, Badu, A. Ayew; J. Ayew, Gyan
REFA:Koman Coulibaly [Mali]

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top