MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza
kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupigwa.
Mechi ya mapema itawakutanisha KMKM dhidi ya Mtende
kuanzia majira ya saa 9:00 alasiri.
Mechi ya pili itaanza majira ya saa 11:00 jioni
ambapo mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc watashuka dimbani kuoneshana
kazi na mabingwa watetezi wa kombe hilo, KCC ya Uganda.
Hii itakuwa mechi kali kutokana na upinzani wa
timu hizi mbili na ikizingatiwa juzi juzi zilikutana nchini Uganda katika mechi
ya kirafiki ambapo Azam fc ilitandikwa mabao 3-2.
Usiku majira ya 2:00, Yanga itashuka dimbani
kuchuana na Taifa ya Jang’ombe.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm pamoja na
msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa jana walikuwepo uwanja wa Amaan Zanzibar
kushuhudia mahasimu wake Simba wakichuana vikali na vinara wa ligi kuu soka
Tanzania bara, Mtibwa Sugar FC.
Katika mchezo huo bao pekee la Henry Joseph Shindika lilitosha kuwaliza Simba 1-0.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni