STEVEN GERRARD ATANGAZA KUONDOKA LIVERPOOL MWISHONI MWA MSIMU HUU BAADA YA KUDUMU KWA MIAKA 26
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu liverpool kwa kipindi cha miaka 26.
Gerrard alijiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 8 mnamo mwaka 1987 na mpaka kufikia mwaka 1998 alipandishwa timu ya wakubwa na kuitumikia hadi msimu huu aliotangaza kuondoka Liverpool.
Gerrard alizaliwa mwaka 30 May 1980 na sasa ana miaka 34 katika mji wa Whiston, Merseyside,nchini England ameichezea Liverpool mechi 691 na kufunga magoli 177 na kuwa viungo wachache waliofunga magoli zaidi ya 100 kwenye timu zao pia amechezea timu ya taifa mechi 114 na kufunga magoli 21 huku pia akitundika daluga kuchezea timu ya taifa mwaka jana mara baada ya kombe la dunia huku timu yake ikiishia hatua ya makundi.
Gerrard anafahamika kama Captain Fantastic atakumbukwa na wapenzi wa Liverpool kwa kuiongoza timu hiyo kutwaa mataji mbalimbali hasa lile la Uefa Champions League mwaka 2005 kwa kuifunga AC Milan kwa mikwaju ya Penalty.
Bado Gerrard hajaweka wazi atakwenda timu gani lakini vilabu kadhaa vya nchini Marekani vimeanza mazungumzo nae lakini LA Galaxy ndio inaonekana kuwa kifuambele kuwania saini ya mkongwe huyo ila Gerrard amesema atatangaza baadae kama atakwenda wapi.
REKODI ZA GERRARD LIVERPOOL
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni