LOGO




LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko Anfield kwa Bigi Mechi kati ya Liverpool na Vinara wa Ligi Chelsea.
Mechi hii, itakayoanza Saa 9 Dakika 45 Mchana, inazikutanisha Liverpool, walio Nafasi ya 7 kwenye Ligi, na Vinara wa Ligi Chelsea walio Pointi 12 mbele yao.
Timu zote hizi mbili zinatoka kwenye Mechi za kati Wiki za UEFA CHAMPIONZ LIGI wakati Liverpool, ikipumzisha Mastaa wao kibao, ilifungwa 1-0 huko Spain na Mabingwa wa Ulaya Real Madrid na Chelsea kucheza ugenini huko Slovenia na kutoka 1-1 na NK Maribor.
Kwenye Ligi, Wikiendi iliyopita, Liverpool ilichapwa 1-0 na Newcastlle na Chelsea kuifunga QPR Bao 2-1.
Msimu uliopita, kwenye Mechi kama hii, Chelsea iliitwanga Liverpool Bao 2-0.
Mara baada ya Bigi Mechi hii, zitafuata Mechi 4 zitakazoanza Saa 12 Jioni na mojawapo ni kule Old Trafford ambapo Man United, ambao Wikiendi iliyopita walichapwa 1-0 na Man City, watacheza na Crystal Palace iliyofungwa 3-1 na Sunderland.
Mechi ya mwisho Jumamosi ni ile itakayoanza Saa 2 na Nusu Usiku huko Loftus Road ambako QPR itacheza na Mabingwa wa England Man City ambao Juzi kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, wakicheza kwao Etihad, walinyukwa 2-1 na CSKA Moscow.
Jumapili Ligi itaendelea kwa Mechi nne.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 8
1545 Liverpool v Chelsea
1800 Burnley v Hull
1800 Man United v Crystal Palace
1800 Southampton v Leicester
1800 West Ham v Aston Villa
2030 QPR v Man City
MSIMAMO
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
10
16
26
2
Southampton
10
16
22
3
Man City
10
10
20
4
Arsenal
10
7
17
5
West Ham
10
5
17
6
Swansea
10
3
15
7
Liverpool
10
0
14
8
Tottenham
10
-1
14
9
Everton
10
2
13
10
Man United
10
2
13
11
West Brom
10
0
13
12
Newcastle
10
-4
13
13
Stoke
10
-2
12
14
Hull
10
-1
11
15
Sunderland
10
-7
11
16
Aston Villa
10
-11
10
17
Crystal Palace
10
-5
9
18
Leicester
10
-5
9
19
QPR
10
-11
7
20
Burnley
10
-14
4

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top