STRAIKA wa Klabu ya Yanga, Mrisho
Ngassa, ameingia kwenye Rekodi rasmi za Afrika baada ya kuibuka kuwa Mfungaji
Bora wa CAF CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2014 akiwa na Bao 6 akifungana na Wachezaji
wengine Watatu.
Wengine waliofunga Bao 6 kwenye
Mashindano hayo ambayo ES Setif ya Algeria iliibuka kuwa Mabingwa ni El Hedi
Belameiri wa Setif, Firmin Ndombe Mubele wa AS Vita ya Congo DR na Haythem
Jouini wa Esperance ya Tunisia.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mtanzania
kuingia kwenye Chati aina hii kwenye Mashindano ya Barani Afrika.
CAF CHAMPIONZ LIGI 2014
WAFUNGAJI BORA:
Wote Bao 6
-Mrisho Ngasa [Yanga, Tanzania]
-Haythem Jouini [Espérance
Tunis]
-Firmin Ndombe Mubele [AS Vita,
Congo
DR]
-El Hedi Belameiri [ES Setif,
Algeria]
Ngassa alifunga Bao zake zote 6
dhidi ya Komorozine ya Visiwa vya Comoro waliyokutana nayo Raundi ya Awali ya
CAF CHAMPIONZ LIGI mapema Mwaka huu.
Kwenye Mechi ya kwanza Jijini Dar es
Salaam Ngassa alipiga Bao 3 Yanga waliposhinda 7-0 na marudiano huko Comoro,
Ngassa tena alipiga Hetitriki Yanga ikishinda 5-1.
Raundi iliyofuata Yanga walikutana
na waliokuwa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri na kubwagwa nje.
Ngassa, mwenye Miaka 25, Mwaka 2009
aliwahi kwenda kufanya majaribio huko England na Klabu ya West Ham na vile vile
huko Marekani na Klabu ya Seattle Sounders Mwaka 2011 na kucheza Mechi dhidi ya
Manchester United waliyofungwa 7-0.
Hapa Nchini pia ameshazichezea Klabu
za Kagera Sugar, Azam FC na Simba.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni