MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal amesema inaweza kuchukua hata Miaka Mitatu kuijenga upya ifikie ilipokuwa kabla ya sasa.
Baada ya Mechi 10 za Ligi, Man United wameambua Pointi 13 na ni mwanzo mbovu kwao tangu Msimu wa 1986.
Van Gaal amenena: “Sio nzuri. Lakini tangu mwanzo nilisema tuko kwenye mchakato. Utachukua zaidi ya Mwaka, utachukua Miaka Mitatu!”
Lakini kazi ya Van Gaal imekuwa ngumu kupita kipimo baada ya kukumbwa na majeruhi wengi hasa kwenye Difensi na kuna wakati kulazimika kuchukua Chipukizi toka Timu ya Rizevu kina Blackett na Paddy McNair.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni