Siku chache kabla ya dirisha dogo
dirisha dogo la usajili, Azam FC imefunguka kuwa ipo tayari kuwauza
wachezaji wake Shomari Kapombe, Kipre Tchetche na Mwadini Ali endapo
kutatokea klabu nyingine inayoweza kutoa dau zuri.
Hatua hiyo inakuja hivi karibuni, baada
ya kuripotiwa kuwa Kipre anaweza kuondoka klabuni hapo kuelekea nchini
Malaysia, Sri Lanka au katika Klabu ya Sofapaka ya nchini Kenya.
Katibu Mkuu wa Azam FC amesema, Idrissa
Nassor, alisema kuwa kama kuna timu itawahitaji wachezaji wao watawauza
lakini kwa dau la uhakika kutokana na viwango vyao.
Nassor alisema kuwa mpaka sasa hakuna
mchezaji wa kikosi hicho ambaye amemaliza mkataba wake ili kuweza
kuondoka katika klabu hiyo labda mpaka pale msimu utakapokuwa
unamalizika.
“Kama kuna timu yoyote ya ndani au nje
itawahitaji wachezaji wetu kama Kipre Tchetche, Shomari Kapombe au
Mwadini Ali hatuna tatizo, kikubwa ni maelewano, ingawa wachezaji hawa
wana mkataba,” alisema Nassor.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
ZILIZOSOMWA SANA
-
MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupig...
-
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu liverpool kwa kipindi cha mi...
-
Siku kadhaa baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya Miss Tanzani...
-
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko...
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni