LOGO

Tokeo la picha la yanga 2-1 kagera sugar
Yanga imefanikiwa kurudi kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kuwachapa Kagera Sugar bao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini dare es Salaam.

Yanga imefikisha point 62 sawa na wapinzani wao Simba SC lakini Yanga inakaa kileleni ikiwa na idadi nzuri ya magoli ya kufunga huku ikiwa na mchezo mmoj mkononi.

Mchezo huo uliathiriwa na mvua zinaezoendelea kunyesha lakini Saimon Msuva aliwafungua Yanga goli la ufunguzi kabla ya Mbaraka Yusuph kusawazisha na kufanya timu hizo kwenda mapumziko wakiwa wamefungamna goli 1-1.

Kipindi cha Pili Mzambia Obrey Chirwa aliwapitia goli la pili na la ushindi na mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga walitoka kifuambele kwa kuinyuka Kagera Sugar inayofundishwa na Meki Mexime 

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top