LOGO

Tokeo la picha la yanga sc
Mabingwa wa tetezi wa LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga SC leo inatarajiwa kushuka dimbani kupambana na Kagera Sugar ya mkoani Kagera katika mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom, mechi nyingine mbili zitachezwa Ijumaa Mei 12, 2017 ambako Simba SC itaialika Stand United FC ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC siku hiyo hiyo ya Mei 12, mwaka huu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Jumamosi Mei 13, mwaka huu JKT Ruvu itakuwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kucheza na Majimaji ya Songea wakati Tanzania Prisons itaikaribisha Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu ulioko Mvomero, Morogoro huku Mbeya City ikisafiri hadi Dar es Salaam kucheza na Young Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top