LOGO

 
AFRICAN SPORTS ILIZALIWA MNAMO MWAKA 1932 JIJINI TANGA KATIKA MAENEO YA BARABARA 12 HUKU IKIJULIKANA KAMA WANA KIMANUKIMANU.

HUKU WAASISI WAKE WAKIWA NI MOHAMEDI MSUO, MAJITU HUKU WOTE WAKIWA NI MAREHEMU NA MUANZILISHI ALI HAI MPAKA SASA NI ATHUMANI MAKALO.
HUKU WACHEZAJI WALIOTAMBA NA KIKOSI HICHO MIAKA HIYO WALIKUWA NI MAKIPA MOHAMEDI YAHAYA, OMARI MAHADHI MABEKI NI MWERI SIMBA, OMARI ZIMBWE,SALIM KIJEMBE, OMARY MWABUIDA HUKU KIUNGO NI AMRAN SHIBA
KATIKA MWAKA AMBAO HAUTASAHAULIKA KWA AFRICA SPORTS NA WENYEJI WA TANGA NI MWAKA 1988 AMBAPO MATAJI MAWILI MAKUBWA NCHINI TANZANIA YOTE YALITUA TANGA KWA KLABU ZA AFRICAN SPORTS NA COASTAL UNION.


COASTAL UNION WAKIBEBA UBINGWA WA TANZANIA BARA HUKU WANA KIMANUMANU AFRICAN SPORTS WAKITWAA TAJI LA MUUNGANO AMBALO NDIO LILIKUWA LENYE HESHIMA KUBWA ZAIDI WAKATI HUO AMBALO LILISHIRIKISHA TIMU ZA TANZANIA BARA NA TANZANIA VISIWANI HUKU PIA KOMBE HILO LA MUUNGANO LIKITOA WAWAKILISHI WA MICHUANO YA AFRICA.


HUKU BINGWA WA TANZANIA BARA AKIPATA NAFASI YA KUSHIRIKI KOMBE LA AFRICA MASHARIKI NA KATI GOSAJE CUP NA SASA NI KAGAME CUP


KIKOSI HICHO CHA UBINGWA MWAKA 1988 KILIUNDWA NA SALIM WAZIRI, BAKARI TUTU, FRANSIS MANDOZA, HASANI BANDA, MHANDO MDEVI, RAPHAEL JOHN, ABAS MCHEMBA, TWAHA OMARI,VICTOR MKANWA, MCHUNGA BAKARI NA JUMA BURHANI
HUKU WACHEZAJI WA AKIBA NI DUNCAN MWAMBA, MARTIN MAHIMBO,ABDUL MOHAMEDI, ABDUL AHMED BOSNIA, HAMZA MANENO, DADI FARES NA WENGINE WENGI HUKO MAKOCHA WAKIWA SILA SAIDI MZIRAY SUPER COACH MAREHEMU PAMOJA NA MUHAJI MWABUDA.


KWA KUNYAKUA UBINGWA HUO WA MUUNGANO AFRICAN SPORTS ILIPATA NAFASI YA KUIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRICA KATIKA MCHEZO WA KWANZA IKINYINYUKWA MAGOLI 2-0 UGENINI NA NA MCHEZO WA MARUDIANO HAUKUCHEZWA KWA SABABU SHIRIKISHO LA MPIRA NCHI TANZANIA WAKATI HUO LIKIITWA FAT LILIKUWA NA MADENI CAF NA KUSABABISHA WAPINZANI WAO KUPITA KWA MAGOLI YA MEZANI.


BAADA YA KIPINDI HICHO CHA MAFANIKIO KWA AFRICAN SPORTS MIAKA MITATU BAADAE YANI MWAKA 1991 KWA MSAHANGAO WA WENGI TIMU HIYO ILITEREMKA RASMI DARAJA LA LIGI KUU HADI LIGI DARAJA LA PILI WALIMU WENYE HESHIMA NCHINI KAMA BONIFACE MKWASA MASTER PAMOJA NA FREDDY FELIX MINZIRO WALIJARIBU KUIRUDISHA TIMU HIYO LIGI KUU BILA MAFANIKIO.


IMEBIDI KUSUBIRI KWA MIAKA 23 WAPENZI NA MASHABIKI WA AFRICAN SPORTS KUIONA LIGI KUU KUTOKA MWAKA 1991 HADI MWAKA 2015 AMBAPO MAKOCHA WALIOIRUDISHA AFRICAN SPORTS LIGI KUU NI JOSEPH LAZARO BEKI WA ZAMANI WA COASTAL UNION NA YANGA SC NA KASSIMU MWABUDA HUKU KOCHA WA WALINDA MLANGO NI ABDUL MGUTO CHINI YA MENEJA ABDUL AHMED MOHAMED BOSNIA
HUKU WACHEZAJI NI YUSUFU ABDUL, HALFANI TWENYE, MUSSA AJIRAN, JUMA SHEMVUNI, MWAITA NGEREZA, SULTAN JUMA, RAMADHANI HAMIDU, ALLY RAMADHANI NA ALLY SHIBOLI


WENGINE NI JAMES NYENDI, NYANZA KAZYOBA, TOKALA NZAU, AYUBU MASOUDI, ALLY ISSA, MUSSA CHAMBE, ALLY AHMEDI, FADHILI KIZENGA, EVRASTUS MUJWAHUKI, FADHILI ABAS, NZARA NDARO, RASHID ALLY, HUSSSENI ISSA, ZAKARIA MAJALIWA, ISSA YASSINI PAUL MUNA, MOHAMEDI RASHIDI, KASSIMU JUMA. HAO WOTE WAKIWA NI VIJANA WADOGO NA WENYE VIPAJI VYA HALI YA JUU,


KUPANDA KWA AFRICAN SPORTS LIGI KUU KUMEKUJA KUTOKANA NA UMOJA WA WAKAZI WA TANGA KATIKA KUISAPOTI TIMU HIYO HADI INAFANIKIWA KUCHEZA LIGI KUU KWA MARA YA KWANZA KWA KIPINDI CHA MIAKA 23.
 

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top