Leo katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki ktk ajali. Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole.
Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema watapaswa kutokuongea, nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mhe.Ole Nasha, nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais hasingeweza kukubaliana na ujinga huu.
Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani, jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya salamu za rambi rambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki, mambo yalibadilika nailionekana dhairi kuwa sitakiwi kabosa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na msiba huu mbaya.
Mkiti Mbowe aliandika meseji kwenda kwa M/ Rais kukumbusha umujimu wa wenyeji kutoa salamu, Makamu wa Rais baada ya kupokea meseji hiyo, alimwita Mkuu wa Mkoa, ndipo ilionekana kama kuna ushindani unatokea kati yao, lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa salamu kwa wapendwa wetu.
Wabunge wa CCM waliokuwepo (ambao wote ni mawaziri) waliweza kutoa pole. Huu ni ubaguzi uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa, nitauleza madhara yake kwenye hotuba yangu kesho. Lakini nafikiri watoto wanafuata walichofundishwa na wazazi. Pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais. Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama Nchi na Syria ni wakati.
Nawashukuru wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha, Mungu awabariki sana. Msiogope, Mungu hadhihakiwi. Apandacho Mtu ndicho atakachovuna.!
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni