
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia
raundi ya 12 wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Januari 24 mwaka huu)
kutakuwa na mechi kati ya Polisi Morogoro na Yanga kwenye Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Mechi
za Jumapili ni kati ya Azam na Simba (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar na
Ndanda (Uwanja wa CCM Kirumba), Stand United na Coastal Union (Uwanja
wa Kambarage),, Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Ruvu
Shooting na Mtibwa Sugar (uwanja wa Mabatini), na JKT Ruvu na Mgambo
Shooting (Uwanja wa Azam Complex).
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni