LOGO

Na Nasri Kitwana.

Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone amesema yeye hawezi kumzuia mchezaji yoyote wa timu yake kuondoka ndani ya timu hiyo endapo atapata sehemu nyingine ya kwenda. Simeone aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la L'Equipe kuhusu hatma ya Antoine Griezman ambaye amekuwa akihusishwa na kutimka ndani ya miamba hiyo ya mjini Madrid na timu kadhaa ikiwemo Manchester United, Barcelona na PSG zinahusishwa  kumnyakua mfaransa huyo.
 Akizungumza katika mahojiano hayo Simeone amesema ''Griezman anaweza kuondoka kama ilivyotokea kwa Diego Costa na Arda Turan pale walipoondoka''. Simeone ameongeza kuwa furaha yake ni kuwaona wachezaji wake wakifanikiwa zaidi hivyo pale mchezaji anapopata mahali sahihi pa kwenda yeye hawezi kumzuia. Griezman ambaye mkataba wake unafikia kikomo 2022 timu itakayohitaji kumnunua mchezaji huyo italazimika kutoa kitita cha euro millioni 100.
 Siku za hivi karibuni wachezaji wengi wa Atletico Madrid wamekuwa wakihusishwa kuihama timu hiyo ambapo beki wa kulia wa timu hiyo Sime Vrsaljko anahusishwa na kujiunga na Napoli katika dirisha la usajili mwezi January ambapo Simeone amesema suala la kusajili na kuuza wachezaji ni suala la kawaida katika soka.

Next
This is the most recent post.
Previous
Taarifa za zamani

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top