
Miamba ya soka nchini Spain clabu ya Real Madrid imefanikiwa kushinda taji la dunia kwa ngazi ya klabu baada ya kufanikiwa kuichapa timu ya San Lorenzo ya nchini Argentina kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa katika dimba la Marrakesh Stadium nchini Morocco

Mabingwa hao wa Ulaya pia wanafundishwa na Carlo Anceloti walijipatia bao la kuongoza kupitia kwa beki wake Sergio Ramos katika dakika ya 37 ya mchezo huo ambapo mpaka mapumziko Madrid walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 kwa sifuri.
Gareth Bale aliwahahakikishia ushindi Madrid kwa kufunga goli la pili katikadakika ya 57 ya mchezo huo ambapo yalidumu mpaka dakika ya 90 ya mchezo huo.
Ushindi huo umefanya Madrid kucheza mechi ya 22 bila kupoteza katika mashindano yote, Cristiano Ronaldo na Kroos wanaweka historia ya kuwa wachezaji pekee walioshinda taji hilo mara mbili wakiwa na vilabu viwili tofauti Ronaldo alitwaa mwaka 2009 akiwa na Man utd na Kroos alishinda taji hilo mwaka 2013 akiwa na Bayern Munich.
Ni Miaka 12 sasa tangia Real Madrid washiriki michuano ya dunia kwa ngazi ya klabu na inakuwa ni mara ya kwanza kwa Madrid kushinda taji hilo.

VIKOSI
Real Madrid: Casillas,
Carvajal (Arbeloa 73), Pepe, Sergio Ramos (Varane 89), Marcelo (Fabio
Coentrao 44), Ronaldo, Kroos, Rodriguez, Bale, Isco, Benzema.
Goals: Sergio Ramos 37, Bale 51.
San Lorenzo:
Torrico, Yepes (Cetto 61), Mas, Kannemann, Mercier, Buffarini,
Kalinski, Barrientos, Ortigoza, Cauteruccio Rodriguez (Matos 68), Veron
(Romagnoli 57).
Referee: Walter Lopez (Guatemala).
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.