Hali za Timu
Liverpool inayonolewa na Brendan Rodgers itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya mchezo uliopita kwa kuchapwa magoli 3-0 na Manchester United katika uwanja wa Old Traford huku Arsenal inyokochiwa Arsene Wenger itaingia uwanjani ikiwa kumbukumbu nzuri ya kuifunga Newcastle United magoli 4-1 wikiend iliyopita.
Timu zote bado hazijakaa sawa katikamsimamo wa ligi huku Liverpool ikishika nafasi ya 11 kwa kuwa pointi 21 na Arsenal ikishika nafasi ya 7 kwa kuwa na pointi 26
Liverpool wanasubiri tathmini ya Beki wao Dejan Lovren ambae ana maumivu ya nyonga aliyopata Jumatano kwenye Mechi ya Robo Fainali ya Capital One Cup ambayo waliichapa Bournemouth.
Ikiwa Lovren hatacheza, nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Mamadou Sakho.
Liverpool itamkosa Straika wao Mario Balotelli ambae amefungiwa Mechi moja.
Arsenal inabidi wawafanyie tathmini Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain na Nacho Monreal ikiwa wako fiti kucheza Mechi hii lakini wanae Beki Calum Chambers ambae amerejea baada ya kumaliza Kifungo chake.
Majeruhi wa Arsenal ambao wataikosa Mechi hii ni Laurent Koscielny, Mikel Arteta, Mesut Ozil, David Ospina, Abou Diaby, Jack Wilshere, Tomas Rosicky na Serge Gnabry.
Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii Uwanjani Anfield, Liverpool iliisambaratisha Arsenal kwa kuitandika Bao 5-1 kwa Bao 2 za Martin Skrtel, 2 za Raheem Sterling na moja la Daniel Sturridge.
VIKOSI VITATOKANA NA:
Liverpool: Jones, Toure, Skrtel, Sakho, Henderson, Gerrard, Lucas, Lallana, Markovic, Coutinho, Sterling, Mignolet, Manquillo, Moreno, Can, Allen, Lambert, Borini. Arsenal: Szczesny, Gibbs, Debuchy, Mertesacker, Monreal, Bellerin, Flamini, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Sanchez, Welbeck, Giroud, Martinez, Podolski, Campbell, Coquelin, Walcott, O'Connor, Maitland-Niles, Ajayi, Akpom.
REFA: Michael Oliver
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.