Jumapili Desemba 21
Newcastle 0 Sunderland 1
Liverpool 2 Arsenal2
Liverpool,
wakicheza kwao Anfield, wamelazimisha sare ya magoli 2-2 dhidi ya Arsenal baada ya kusawazisha bao katika Dakika
ya 96 walipokuwa nyuma kwa Bao 2-1 walipocheza na Arsenal na Refa
Michael Oliver kuongeza Dakika 9 za nyongeza kufidia muda ambao Beki wao
Martin Skrtel alipokuwa akitibiwa na ni yeye Skrtel ndie alisawazisha
Bao hilo kwa Kichwa.
Liverpool walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 45 kupitia
Phillippe Coutinho na Arsenal kusawazisha Dakika moja baadae kwa Bao la
Mathieu Debuchy.
Kipindi cha Pili, Olivier Giroud aliipa Arsenal Bao la Pili na
lilidumu hadi Dakika ya 90 ambapo Refa Michael Oliver aliongeza Dakika 9
za Majeruhi na Dakika 3 baadae Liverpool kubaki Mtu 10 baada ya Fabio
Borini kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kumchezea Rafu Cazorla.
Zikiwa zimebaki Dakika 3 za muda wa Majeruhi uliongezwa kwa kuumia Sentahafu wa Liverpool Martin Skrtel, Beki huyo huyo ndie alieunganisha Kona ya Adam Lallana kwa Kichwa na kuipa Liverpool Sare ya Bao 2-2.
Matokeo haya yamewaacha Liverpool wakiwa Nafasi ya 10 wakiwa na
Pointi 22 huku Arsenal wakiwa Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 27 na Timu
zote zikibaki kutupwa mbali kidogo na Timu 4 za juu ambapo Timu iliyo
Nafasi ya 4, West Ham, ina Pointi 31.
Ligi Kuu England itaendelea Jumatatu Usiku wakati Vinara wa Ligi
Chelsea watakapotembelea Britannia Stadium kucheza na Timu ngangari
Stoke City.
VIKOSI:
Liverpool: Jones; Toure, Skrtel, Sakho; Henderson, Lucas, Gerrard, Markovic; Coutinho, Sterling, Lallana
Akiba: Jose Enrique, Lambert, Moreno, Manquillo, Mignolet, Can, Borini.
Arsenal: Szczesny; Debuchy, Chambers, Mertesacker, Gibbs; Flamini, Oxlade-Chamberlain; Sanchez, Cazorla, Welbeck; Giroud
Akiba: Podolski, Walcott, Monreal, Martinez, Campbell, Coquelin, Maitland-Niles.
MAGOLI:
Liverpool 2
Liverpool 2
-Phillippe Coutinho Dakika ya 45
-Martin Skrtel 90 +6:05
Arsenal 2
-Mathieu Debuchy Dakika ya 45 +1:07
-Olivier Giroud 64
REFA: Michael Oliver
Arsenal defender Per Mertesacker attempts to block
the ball as Coutinho rifles his shot low and hard at goal to fire
Liverpool ahead
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni