BODI ya ligi ya Vodacom Tanzania bara TPLB imezitaka
klabu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza kuendana na kalenda ya
usajili ili kuepusha usumbufu wa kugombania mchezaji
BODI ya ligi ya Vodacom Tanzania bara TPLB imezitaka klabu za ligi
kuu na ligi daraja la kwanza kuendana na kalenda ya usajili ili kuepusha
usumbufu wa kugombania mchezaji kama ilivyowahi kutokea siku za nyuma.Afisa Mtendaji mkuu wa TPLB, Boniface Wambura ameiambia Goal, tayari wametoa kalenda ya usajili na kuanza kwa ligi kuu, hivyo klabu ziwape fursa makocha kusajili wachezaji wanaowataka ndani ya muda uliotangazwa, wakati wao wanaendelea na maandalizi mengine ikiwemo kukagua viwanja na kuzungumza na wadhamini.
“Maeneo mengine ambayo Bodi inafanyia kazi ni maandalizi ya kukagua viwanja vitavyotumika pamoja na ‘Physical fitness test’ na semina kwa waamuzi na makamishina, amesema Wambura.
Wambura amesema hayo ni baadhi ya maeneo ambayo wanayafanyia kazi, lakini wanavisisitiza vilabu kufanya usajili kwa makini kwasababu linakuwa na matatizo.
Timu zinazo shiriki ligi kuu na ile ya Daraja la kwanza zinatumia usajili wa mtandao, kuna timu zimepanda na zinahitaji mafunzo kwa ajili ya usajili wa mtandao tumejipanga kwa ajili ya kuzipa mafunzo ili ziweze kwenda na mfumo huo unaotumika kwa sasa duniani kote.
CHANZO GOAL.COM
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni