Taifa Stars yarejea Bongo
Kwa muda mrefu Stars haijapata matokeo mazuri kwenye mechi za kimataifa
TIMU ya taifa, ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imerejea Dar es Salaam leo ikitokea Misri ambapo Jumapili ilikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwe wenyeji Misri katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika zitakazo fanyika Gabon 2017.
Stars inayofundishwa na kocha Mart Nooij, ilifika uwanjani hapo na kukuta mapokezi mabaya kutoka kwa Watanzania wachache ambao huku wengine wakiwazomea kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo tangu ilipoanza kufundishwa na Mdachi huyo.
Nahodha wa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ameiambia Goal mchezo ulikuwa mgumu na sababu kubwa ni kutokana na ubora wa timu waliyocheza nayo Misri .
“Nimatokeo mabaya kwetu na Watanzania wote lakini hatuna budi tukubali kuwa wenzetu wana timu nzuri hivyo nasisi tutumie kipindi hiki kujipanga vizuri kabla ya kucheza na Nigeria Septemba,”amesema Cannavaro.
Kwa muda mrefu Stars haijapata matokeo mazuri kwenye mechi za kimataifa hali iliyofanya jana wachezaji wake kutoka uwanjani kwa mafungu huku wengine wakikwepa kuzungumza na vyombo vya habari.