Mabingwa wa ligi kuu ya
Uingereza, klabu ya Chelsea, inatarajia kutumia uwanja wa Wembley kwa
muda ili kupisha marekebisho ya uwanja wao wa Stamford Bridge.
Chelsea itapewa uwanja wa Wembley
kama itakidhi vigezo vilivyotolewa na uongozi husika wa uwanja huo
ikiwemo kuhakikisha mashabiki watakaoingia uwanjani hawapungui elfu 50.
Mchakato wa marekebisho ya Stamford Bridge yalianza mwaka mmoja uliopita
chini ya mmiliki wa klabu hiyo Roman Ibramovich, lengo kuu likiwa ni
kuongeza viti ili kuruhusu mashabiki wengi kuingia na kuongeza mapato
tofauti na ilivyo sasa ukiwa unaingiza mashabiki elfu 41 tu.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni