Klabu ya Ac Milan imethibitisha
kumtimua kocha wake, Filippo Inzaghi baada ya kuwa na msimu mbaya
katika ligi ya Serie A na nafasi yake inachukuliwa na Sinisa Mihajlovic.
Mihajlovic ambaye alikuwa kocha
wa Sampdoria msimu uliopita, amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa
kikosi hicho na atalipwa karibia paundi milioni 2.5 kwa msimu.
Licha ya kumtimua kocha huyo AC Milan wamempongeza kwa kazi yake aliyoifanya akiwa kwenye klabu hiyo.
Ac Milan chini ya Inzaghi
imemaliza msimu uliopita ikiwa imeshika nafasi ya kumi ikijikusanyia
52, wakati Mrithi wake Sinisa alimaliza nafasy ya 7 akiwa na Sampdoria.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni