Kocha
mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema, amefurahia ujio wa
mshambuliaji Ame Ali kwenye kikosi chake na hana wasiwasi naye.
Ame ni mchezaji pekee aliyesajiliwa na Azam msimu huu akitokea Mtibwa Sugar na ujio wake, ulibarikiwa na Stewart mwenyewe.
"Ame
ni mchezaji mzuri, namjua na nilikuwa nikimfuatilia alipokuwa
anaichezea Mtibwa. Naamini uwepo wake utaisaidia Azam msimu huu,"alisema
Stewart.
"Alipendekezwa
kwa mujibu wa ripoti iliyopita na kabla ya kusajiliwa, uongozi
uliniuliza kwanza kama atanifaa na mimi niliwajibu sawa, wakakamilisha
mipango."
Hata
hivyo, Ame bado hajaanza mazoezi na Azam, yuko kwao Zanzibar, alirudi
mara tu aliposaini mkataba huo kwa ajili ya kujipanga zaidi.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni