MSHAMBULIAJI Amme Ally Amour
aliyetamba na kikosi cha Mtibwa Sugar msimu uliopita, ameripotiwa
kukamilisha taratibu za kujiunga na makamu bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL) kwa mkataba wa miaka miwili.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC,
Saad Kawemba, amekaririwa na mtandao wa Goal.Com akieleza kuwa
wamemsajili Amme ili kuiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji ambayo
msimu uliopita ilikuwa ikimtegemea zaidi Mrundi Didier Kavumbagu
aliyefunga mabao 10 na kuwa kinara wa mabao kwa timu hiyo.
“Tunashukuru kwa kufanikisha
dili hili, Amme ni mtu sahihi kwetu ndiyo sababu tunataka kuwa naye.
Tunaamini atafanya kazi yake kama alivyokuwa Mtibwa na kutupa taji la
Tanzania Bara,” amekaririwa Kawemba.
Amme aliyefunga mabao nane
msimu uliopita kabla ya kutua Azam alikuwa akiwaniwa na klabu ya Simba
ambayo inahaha kutafuta mshambuliaji atakayeziba pengo la Danny
Sserunkuma aliyesitisha mkataba na timu hiyo na kurudi kwao Uganda.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni