Manchester United imeanza mwaka vibaya kwa kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Stoke City katika mchezo wa ligi kuu nchini England uliopigwa kwenye uwanja Britania Stadium.
Wenyeji Stoke City ndio waliotangulia kufunga baada ya Dakika 2 tu baada ya Kona yao kuunganishwa kwa Kichwa na Peter Crouch na Mchezaji wa zamani wa Man United Ryan Shawcross kuutumbukiza Mpira wavuni.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 26 kufuatia Kona ya Nahodha Wayne Rooney kuparazwa kwa Kichwa na Michael Carrick na Radamel Falcao kuunganisha Mpira wavuni.
Kipindi cha Pili hakikuzaa Bao zozote licha ya nafasi kadhaa hasa kwa Stoke ambao Straika wao Peter Crouch alipiga Kichwa na kugonga mwamba na kuokolewa.
Matokeo haya yameibakisha Man United Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 37.
VIKOSI:
Stoke City: Begovic; Cameron, Shawcross , Muniesa, Pieters; Walters, Nzonzi, Whelan, Arnautovic; Diouf, Crouch
Akiba: Butland, Bardsley, Huth, Wilson, Adam, Assaidi, Shenton.
Manchester United: De Gea; Young, Jones, Smalling, Evans, Shaw; Carrick, Mata, Rooney; van Persie, Falcao
Akiba: Lindegaard, Blackett, Rafael, Fletcher, Herrera, Januzaj, Wilson.
REFA: Michael Oliver
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni