LOGO

andoni
Equatorial Guinea imetangaza kumfukuza kazi kocha wake mkuu wa timu hiyo Andoni Goikoextea huku zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya michuano ya AFCON. 
Equatorial Guinea ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo wamemfukuza kocha huyo raia wa Spain baada ya uchaguzi wa shirikisho la soka la Equatorial Guinea kufanyika ambapo kazi ya kwanza iliyofanywa na uongozi mpya ilikuwa kumfukuza kazi kocha huyo Mhispania .
Rais mpya wa shikisho la soka Equatorial Guinea Andres Jorge Mbomio alithibitisha uamuzi wa kumfukuza Andoni Goikoextea ambaye amekaa na timu ya taifa hilo kwa miaka miwili na hakutaja sababu za msingi za kufukuzwa kwa nkocha huyo hali ambayo inatishia kuvuruga maandalizi ya wenyeji hawa wa Afcon kuelekea kwenye michuano yenyewe .
Wachezaji wa Equatorial Guinea wakishangilia goli kwneye michuano ya AFCON 2012.
Wachezaji wa Equatorial Guinea wakishangilia goli kwneye michuano ya AFCON 2012.
Hata hivyo inadaiwa kuwa kiwango duni ambacho Equatorial Guinea imekionyesha kwenye mechi mbili za kirafiki dhidi ya Kikosi B cha klabu ya Benfica na Villafranquense huko nchini Ureno pamoja na kufanya vibaya kwenye michuano ya WAFU kumeufanya uongozi kukosa Imani naye japo muda uliobaki kuelekea kwenye AFCON.
Kocha Andoni akiwa na mmoja kati ya wachezaji wake kwenye timu ya taifa ya Equatorial Guinea.
Kocha Andoni akiwa na mmoja kati ya wachezaji wake kwenye timu ya taifa ya Equatorial Guinea.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top