LOGO

Mcheza wa Mapinduzi Cup ambao umewakutanisha mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Azam dhidi ya Mabingwa wa Uganda timu ya KCCA umemalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Amani Zanzibar huku timu hizo zikitoshana nguvu kwa magoli 2-2.
Azam walitangulia kufunga mara mbili huku KCCA wakiwa na kazi ya kusawazisha mabao hayo. John Bocco na Salum Aboubakary walifunga kwa Azam huku William na Masiko wakifunga kwa upande wa KCCA.

Mchezo huo ulishuhudia kikosi cha Azam kikiwakosa Kipre Tchetche, Kipre Balou na Didier Kavumbangu ambao ni wagonjwa huku beki David Mwantika kwa mara ya kwanza akicheza sambamba na Agrey Morris kwenye safu ya ulinzi huku beki raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa akianzia benchi.
Katika mchezo huo, kocha Joseph Omog alimtoa mapema kiungo Amri Kiemba kwenye mchezo huo huku KCCA nao wakimtoa Owen Kasule baada ya kuonekana kutokuwa kwenye ubora huku kiungo mshambuliaji mpya wa Azam, Brian Majwega akionyesha kiwango bora kabisa kwenye mchezo huo.
Michezo mingine ya timu kutoka bara ilichezwa jana pale Mtibwa Sugar walipocheza na Simba na kuwalaza bao 1-0 na muda mfupi ujao, timu ya Yanga itashuka dimbani kumenyana na Timu ya Taifa ya Jang'ombe huku mashabiki wa wana Jangwani hao wakiwa na matumaini makubwa na timu yao.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top