SIMBA imempa ruhusa straika wake Emmanuel Okwi
aende kwao Uganda kumalizia fungate yake kama alivyoaga, lakini mchezaji
bado yuko Dar es Salaam huku wenzake wakiwa na timu Zanzibar
wakishiriki Kombe la Mapinduzi.
Usiku wa jana Alhamisi, Simba ilicheza mechi yake
ya kufungua michuano ya hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar bila ya Okwi na
Waganda wenzake; Juuko Murshid na Simon Sserunkuma ambao wametimkia kwao
baada ya kutolipwa fedha zao za usajili.
Uongozi wa Simba unajua kwamba Okwi yupo Uganda lakini ukweli ni kwamba mchezaji huyo yupo Dar es Salaam.
Rafiki wa karibu na Okwi, alilithibitishia
Mwanaspoti kuwa, mchezaji huyo hakwenda Uganda japokuwa aliomba ruhusa
hiyo na viongozi kumruhusu lakini aliamua kufanya hivyo kwa sababu zake
binafsi.
“Okwi ni rafiki yangu mkubwa, ni kweli yupo hapa Dar es Salaam na wala hakwenda Uganda,” alisema.
“Nilimshauri asifanye kwani Simba wamempa fedha nyingi za usajili, kwa nini awasumbue?” alihoji rafiki yake huyo.
Okwi alisaini mkataba mpya wa kuichezea Simba
mwezi uliopita ambapo chanzo hicho kilifafanua kwamba katika fedha ya
usajili, Okwi alipewa dola 30,000 (Sh 50 milioni) wakati anajiandaa
kwenda kwao kufunga ndoa.
“Sijui kama kulikuwa na fedha zaidi ya hizo kwenye
usajili wake kwani ninavyojua ni kwamba alipewa kiasi hicho na kwenda
kwao, labda kama makubaliano ni zaidi ya hapo sijui kwani.MWANASPOTI
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni