
KAZI iliyobaki Msimu huu kwa Borussia Dortmund ni kupigana kutoshuka Daraja licha ya kuwa na matumaini makubwa kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE na German Cup kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wao, Hans-Joachim Watzke.
Dortmund,
ambao Mwaka 2011 na 2012 walikuwa Mabingwa wa Germany na pia Mwaka 2013
kufika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Msimu huu wamekuwa goigoi na
wapo Nafasi ya 17 kwenye Msimamo wa Bundesliga wakiwa na Pointi sawa na
Timu ya mkiani Freiburg.
Watzke ametamka: “Lengo letu ni wazi. Lengo letu ni kubakia Bundesliga!”
Kwenye
Bundesliga, wamefungwa Mechi 10 kati ya 17 na kuzoa Pointi 15 tu lakini
kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE wapo Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Mwezi
ujao wataivaa Juventus.
Ingawa
tayari wameimarisha safu yao ya Kiungo kwa kumsaini Mchezaji wa
Slovenia, Kevin Kampl, anachezea Red Bull Salzburg ya Austria, Watzke
amesema hawatarajii kumchukua Mchezaji mwingine.
Ametamka: “Hatutegemei lakini si kwamba haiwezekani!”
Pia Mkuu huyo wa Dortmund aliwahi kuhakikisha kuwa Kocha wao Juergen Klopp yupo salama licha ya mwendo wa ovyo wa Timu.
Mapema
Mwezi huuWatzke, akiongea na Gazeti la SportBild, alitamka: “Kamwe
hatutamfukuza Juergen Klopp. Ana kila sifa hapa Klabuni. Hatutafikia
kwenye mgogoro!”
Klopp, alijiunga na Dortmund Mwaka 2008.
Hivi sasa Bundesliga ipo kwenye mapumziko ya Krismasi na Mwaka mpya na itarejea dimbani kuanzia Januari 30.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni