
Robin van Persie anatarajiwa kuikosa Mechi ya Ugenini ya Manchester United ya Jumamosi dhidi ya QPR ya Ligi Kuu England kutokana na tatizo la Enka.
Kukosekana kwa Van Persie huenda kukatoa mwanya kwa Radamel Falcao kucheza baada ya kutokuwemo kwenye Kikosi kilichofungwa 1-0 na Southampton katika Mechi iliyopita.
Van Persie aliumia Enka yake kwenye Mechi hiyo hiyo na Southampton Uwanjani Old Trafford na kulazimika kutolewa katika Dakika ya 61.
Hata hivyo, Man United wanategemea Nahodha huyo wa Holland atakuwa fiti kucheza Mechi yao inayofuatia hii ya QPR hapo Ijumaa Januari 23 Ugenini na Cambridge United kwenye Raundi ya 4 ya FA CUP lakini huenda asichezeshwe na Meneja Louis van Gaal kama alivyopumzishwa kwenye Raundi iliyopita ya FA CUP dhidi ya Yeovil Town.
Baada ya kutomweka kabisa kwenye Kikosi cha Mechi na Southampton, Meneja Louis van Gaal alifafanua kuwa uamuzi wake huo ulitokana na sababu za kiufundi na si kutokuwa fiti kwa Falcao.
Uamuzi huo wa kuachwa kwa Falcao ulimkera hata Wakala wake, Jorge Mendes, ambae aliibuka na kusema kuwa hana hakika kama Staa huyo kutoka Colombia atabakia Old Trafford baada ya Mkataba wake wa Mkopo kutoka Monaco kumalizika mwishoni mwa Msimu.
Mkataba huu wa Mkopo unacho kipengele kinachoiruhusu Man United kumnunua moja kwa moja Falcao.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni