LOGO

 
Goli la mfungaji bora wa wakati wote ndani ya Azam FC John Raphael Bocco lilitosha kuwapa pointi moja Azam FC mbele ya yanga sc katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo ambao Azam FC waliuwanza kwa kasi na kufanikiwa kuandika goli katika dakika ya 5 kupitia kwa Didier Kavumbagu, akitumia makosa ya beki ya yanga katika kuuzuia krosi ya Kipre Herman Tcheche.
Goli hilo lilipeleka yanga kuongeza mashambulizi langoni kwa Azam Fc na katika dakika ya 8 Amisi Tabwe aliisawazishia Yanga akiunga mpira wa krosi ulipigwa toka upande wa kulia wa yanga.
Yanga na Azam FC walishambuliana kwa zamu katika kipindi chote cha kwanza na huku makipa wa pande zote mbili wakifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya washambuliaji wapande zote mbili.
Katika kipindi cha pili yanga waliana kwa mabadiliko ya kumuingiza Oscar Joshua na kumpeleka benchi David Charles, mabadiliko yaliyopelekea Yanga kulisakama viliyvo lango la Azam FC.
Kocha Omog alimpumzisha Kipre Tcheche na kumuingiza Amri Kiemba ambaye hakuongeza chochote katika mchezo huo.
Alikuwa Saimon Msuva laiyeipatia Yanga goli la pili katika dakika ya 52 akiunga mpira wa Haruna Niyonzima kwa kichwa.
Kuingia kwa goli hilo kulipelekea kocha Omog kufanya mabadiliko ya kumtoa Salum Aboubakari na kumuingiza John Bocco katika dakika ya 64.
John Bocco aliiandikia Azam FC goli la kusawazisha katika dakika ya 66 akiunga mpira wa Himid Mao na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Baada ya kuingia goli la Bocco yanga walihamisihia makazi katika upande wa Azam FC na kupelekea kutawala mchezo huo na Azam FC kubaki nyuma wakizuia.
MATOKEO MENGINE
FTMTIBWA SUGAR 1 : 1STAND UNITED
FTMBEYA CITY 1 : 0NDANDA
FTPOLISI MORO 2 : 0MGAMBO JKT
FTYANGA 2 : 2AZAM FC

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top