CHELSEA YAPUNGUZWA KASI NA SOTON YATOA SARE YA 1-1
Vinara Chelsea wameambua Pointi 1 Ugenini huko Saint Mary’s Stadium walipotoka 1-1 na Southampton.
Sadio Mane aliipa Southampton Bao la kuongoza na Chelsea kusawazisha Sekunde chache kabla ya Haftaimu.
Southampton walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Morgan Schneiderlin kutolewa kwa Kadi za Nyekundu baada ya Kadi za Njano mbili.
Matokeo haya bado yanawabakisha Chelsea kileleni mwa Ligi mbele ya Timu ya Pili Mabingwa Watetezi Man City ambao hii Leo wanacheza na Burnley na hata wakishinda watakuwa Pointi 1 nyuma ya Chelsea.
VIKOSI:
Southampton: Forster; Alderweireld, Fonte, Yoshida; Tadic, Davis, Schneiderlin, Wanyama, Targett; Mane, Pelle
Akiba: Davis, Gardos, Long, Ward-Prowse, Isgrove, Reed, McCarthy.
Chelsea: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Luis; Matic, Mikel; Schurrle, Fabregas, Hazard; Costa
Akiba: Cech, Zouma, Ramires, Drogba, Remy, Willian, Azpillicueta.
Refa: Anthony Taylor
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni