MANCHESTER UNITED YATOKA SARE NA TOTTENHAM
Manchester United, wakicheza Ugenini huko White Hart Lane Jijini London, walitoka Sare 0-0 na Tottenham na kujichimbia kwenye Nafasi ya 3 ya Ligi Kuu England.
Wakichezesha Kikosi kile kile ambacho hakijabadilika kwa mara ya kwanza baada ya Mechi 85, Man United walikosa Bao za wazi, hasa Kipindi cha Kwanza, lakini Spurs wakaja juu Kipindi cha Pili.
Hii ilikuwa ni Mechi ya kwanza kati ya 9 za Ligi Kuu England ambazo zinachezwa Leo.
VIKOSI:
Tottenham Hotspur: Lloris, Chiriches, Fazio, Vertonghen, Davies, Stambouli, Mason, Townsend, Eriksen, Chadli, Kane.
Akiba: Walker, Paulinho, Soldado, Lamela, Vorm, Dier, Dembele.
Man Utd: De Gea, Jones, McNair, Evans, Carrick, Valencia, Mata, Rooney, Young, van Persie, Falcao.
Akiba: Da Silva, Shaw, Smalling, Lindegaard, Fletcher, Pereira, Wilson.
Refa: Jon Moss
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni