LOGO

RATIBA/MATOKEO:
Saa za Bongo
Jumapili Desemba 28
Tottenham 0 Man United 0                  
Southampton 1 Chelsea 1 
Aston Villa 0 Sunderland 0         
Hull 0 Leicester 1             
Man City 2 Burnley 2                  
QPR 0 Crystal Palace 0               
Stoke 2 West Brom 0                 
West Ham 1 Arsenal 2      
1915 Newcastle v Everton

BPL-2014-2015-LOGO-POAMabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City wameumwaga uongozi wa Bao 2-0 na kuiruhusu Burnley, Timu ambayo iko Nafasi ya Pili toka mkiani, kusawazisha Bao zote na kupata Sare ya 2-2.
City, wakicheza kwao Etihad, waliongoza 2-0 hadi Haftaimu kwa Bao za Daviid Silva na Fernandinho lakini Kipindi cha Pili Burnley walirudisha Bao hizo Wafungaji wakiwa George Boyd na Ashley Barnes.
Matokeo haya yamewabakisha City Nafasi ya Pili Pointi 3 nyuma ya Vinara Chelsea ambao nao mapema hii Leo walitoka Sare 1-1 na Southampton.
Huko Upton Park, Arsenal walitangulia kwa Bao 2-0 kabla ya Haftaimu na kupata ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Wenyeji West Ham ambao walifunga Bao lao moja Kipindi cha Pili Mfungaji akiwa Cheikhou Koiyate.
Ushindi huu umeipandisha Arsenal na kukamata Nafasi ya 5 wakiwa Pointi sawa na Timu ya 4 Southampton ambao wako juu yao kwa ubora wa Magoli.
Timu hizo ziko Pointi 3 nyuma ya Man United ambao wako Nafasi ya 3.
VIKOSI:
Southampton: Forster; Alderweireld, Fonte, Yoshida; Tadic, Davis, Schneiderlin, Wanyama, Targett; Mane, Pelle
Akiba: Davis, Gardos, Long, Ward-Prowse, Isgrove, Reed, McCarthy.
Chelsea: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Luis; Matic, Mikel; Schurrle, Fabregas, Hazard; Costa
Akiba: Cech, Zouma, Ramires, Drogba, Remy, Willian, Azpillicueta.
Refa: Anthony Taylor

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top