LOGO

CAF-LOGO-SAFIHII LEO, CAF imefanya Droo ya Mashindano yake ya Klabu, Caf Champions League na Kombe la Shirikisho kwa Mwaka 2015, ambapo Klabu 4 za Tanzania zitashiriki.
Klabu hizo ni Azam FC, Mabingwa wa Tanzania Bara, na KMKM, Mabingwa wa Zanzibar, ambao watashiriki Caf Champions League wakati Yanga na Polisi ya Zanzibar watacheza Kombe la Shirikisho.
Timu zote hizi 4 zitaanza Raundi za Awali ambazo Mechi zake zitachezwa Wikiendi ya Februari 13, 14 na 15 na Marudio ni Wikiendi ya Februari 27, 28 na Machi Mosi.
Kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI, Azam FC wataanza Nyumbani na Merrikh ya Sudan na Mshindi baada Mechi mbili atatinga Raundi inayofuata kwa kucheza na Mshindi kati ya Lydia Ludic B.A. ya Burundi v Kabuscorp do Plance ya Angola.
KMKM, ambao pia wapo Caf Champions League, wataanza Ugenini kucheza na Hilal ya Sudan na Mshindi wa Mechi zao mbili atacheza na Mshindi kati ya Fomboni Club de Moheli ya Comoro na Big Bullets ya Malawi.
Katika Kombe la Shirikisho, Yanga wataanza Nyumbani na BDF XI ya Botswana wakati Polisi ya Zanzibar itaanza Ugenini na CF Mounana ya Gabon.
Ikiwa Yanga itaibwaga BDF basi watacheza na Mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimbabwe wakati Polisi, wakifuzu Raundi ya Awali, watawacheza na Mshindi kati ya Khartoum ya Sudan na Power Dynamos ya Zambia.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top