Clabu ya Chelsea inayofundishwa na Jose Mourihno imefanikiwa kuichapa timu ngumu ya Stoke City kwa jumla ya magoli 2-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini England EPL kwenye dimba la Britainia Stadium.
Chelsea itakula sikuu ya Christmas ikiwa kileleni mwa msimamao huo baada ya kufikisha point 42 mkononi. Ushindi huo ulianza kupitia kwa nahodha John Terry aliefunga goli la kwanza katika dakika ya 2 ya mchezo huo kufuatia mpira wa kona na kuunganisha kwa kichwa na kufanya chelsea kuomgoza kwa goli 1-0 hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya Stoke City kulisakama lango la Chelsea ambapo walikosa magoli ya wazi huku mabeki na mlinda mlango wa Chelsea wakiokoa hatari hizo.
Huku kila mtu akiamini kuwa mpira utaisha kwa goli 1-0 Cesc Fabregas aliifungia goli la pili Chelsea na la ushindi katika dakika ya 78 ya mchezo huo na kuhitimisha kauli kuwa uwanja wa Britania ni mgumu kwa Vigogo
John Terry rises to beat Geoff Cameron to the ball and give Chelsea the lead after just two minutes at the Britannia Stadium
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni