Baada kuangushiwa kichapo chao cha kwanza kwenye Ligi Kuu England Msimu huu na Newcastle, Vinara wa Ligi hiyo Chelsea walirudi kwa kishindo baada ya Jumatatu kuichapa Stoke City na Ijumaa, Boxing Day, wao ndio watafungua dimba zile Mechi mfululizo kuelekea Mwaka mpya kwa kuwa Uwanjani kwao kucheza na West Ham katika Dabi ya Jiji la London.
Chelsea wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 3 mbele ya Timu ya Pili Mabingwa Watetezi Manchester City na Pointi 10 mbele ya Timu ya Tatu Manchester United ambao wameitangulia Timu ya 4 West Ham kwa Pointi 1.
West Ham, ambao wapo kwa mara ya kwanza katika 4 Bora ya Ligi wakati huu wa Krismasi tangu Mwaka 1985, wanatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Chelsea Uwanjani Stamford Bridge.
Lakini, hata hivyo, matarajio ya West Ham kushinda Mechi hii ni finyu hasa ukiangalia Historia kwani mara ya mwisho kushinda Mechi hii ni Miaka 12 iliyopita ingawa kwenye Mechi kama hii Msimu uliopita waliambua Sare ya 0-0 hapo Stamford Bridge.
Chelsea watatinga kwenye Mechi hii huku kukiwa na wasiwasi kuhusu Mchezaji wao Eden Hazard ambae aliumia enka kwenye Mechi na Stoke ingawa mwenyewe ameripotiwa kudai yuko fiti.
Nao West Ham wanakabiliwa na Majeruhi kwa Wachezaji wao Tomkins na Noble ingawa zipo ripoti kuwa huenda wakawemo Kikosini.
Baada ya Mechi hii, Chelsea Jumapili Desemba 28 watakuwa Ugenini kucheza na Southampton wakati West Ham, Siku hiyo hiyo, wana Dabi nyingine ya London wakiwa Nyumbani Upton Park kwa kucheza na Arsenal.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Willian, Oscar, Schurrle, Costa
Akiba: Cech, Schwarzer, Aké, Filipe Luís, Zouma, Christensen, Mikel, Ramires, Hazard, Drogba, Rémy, Salah
West Ham: Adrian, Jenkinson, Tomkins, Reid, Cresswell, Kouyate, Song, Nolan, Downing, Sakho, Carroll
Akiba: Jaaskelainen, Noble, Collins, O’Brien, Demel, Amalfitano, Poyet, Vaz Tê, Jarvis, Valencia, Cole
REFA: Michael Oliver
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni