LOGO

 
MANCHESTER UNITED ndio Wafalme wa Boxing Day huko England katika Historia ya Ligi Kuu England kwa kuweza kushinda Mechi 19, kupoteza Mechi 1 tu katika Mechi 22 walizocheza Siku hiyo Desemba 26 na safari hii, Siku hiyo hiyo, watakuwa kwao kucheza na Newcastle.
Wakati Man United wakitawala Boksing Dei, Newcastle ni goigoi Siku hiyo kwa kushinda Mechi 4 tu katika Miaka 20 ya Ligi Kuu England na safari hii wanakutana na Man United, ambayo ipo Nafasi ya Tatu kwenye Ligi baada ya wimbi la kutofungwa katika Mechi 7 ambazo wameshinda 6 na Sare 1, wanaoingia Old Trafford wakiwa wamepewa Ofu Siku ya Krismasi na Meneja wao Louis van Gaal kitu tofauti na Timu nyingine ambazo hufanya Mazoezi Siku hiyo kwa ajili ya Mechi za Siku ya Pili.

 DONDOO MUHIMU:
 -Msimu uliopita, Newcastle walishinda kwa mara ya  kwanza Old Trafford tangu Februari 1972.
 -Katika Mechi 30 zilizochezwa Old Trafford, Man United wamefungwa mara 1 tu na Newcastle.
 -Man United hawajahi kufungwa Mechi 2 mfululizo na Newcastle tangu 1935.

Wakiwa na upungufu mkubwa kwenye Difensi, Man United sasa imeanza kuimarika baada ya kupona kwa Jonny Evans na Phil Jones huku Chris Smalling akiwa na nafasi finyu ya kucheza lakini Luke Shaw, Daley Blind na Ander Herrer bado wana maumivu wakati Marouane Fellaini ni mgonjwa.
Kikosi cha Alan Pardew wa Newcastle kitawakosa Kiungo Cheick Tiote ambae yuko Kifungoni na Beki Steven Taylor alieuvaa Mwamba wa Goli kwenye Dabi ya Tyne-Wear walipofungwa 1-0 na Sunderland Wikiendi iliyopita.
Kabla ya Mechi hiyo, Newcastle walicharazwa Bao 4-1 na Arsenal huko Emirates.

MECHI 3 ZILIZOPITA…
-Newcastle 0 Man United 4 (Mata x2, Hernandez, Januzaj), Ligi, Aprili 2014
-Man United 0 Newcastle 1 (Cabaye), Ligi, Desemba 2013
-Man United 4 (Evans, Evra, Van Persie, Hernandez) Newcastle 3 (Perch, Evans Kajifunga, Cisse), Ligi, Desemba 2012

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Man United: De Gea, Jones, Carrick, Evans, Valencia, Young, Mata, Fletcher, Rooney, Van Persie, Falcao
Akiba: Lindegaard, Vermijl, Amos, Thorpe, Rothwell, Anderson, Januzaj, Blackett, McNair, Da Silva, Di María, Lingard, Smalling
Newcastle: Alnwick, Coloccini, Janmaat, Dummett, Williamson, Sissoko, Anita, Colback, Gouffran, Perez, Ameobi,
Akiba: Woodman, Streete, Haïdara, Cabella, Cissé, Rivière, Armstrong, Obertan
REFA: Mike Jones

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top