LOGO

Mzambia Patrick Phiri ameondolewa katika benchi la ufundi la simba sc sambamba na msaidizi wake matola na nafasi zao zitajazwa na aliyekuwa kocha wa Polisi Rwanda, Goran Kopunovic raia wa Serbia.
 
Taarifa zilizotufikha zinaelezaKopunovic anatarajiwa kuwasili nchini siku ya jumatano ya wiki hii, vilevile inaeleza kuwa msaidizi wa kocha huyo atakuwa Jean Marie raia wa Rwanda aliyewahi kufundisha Atraco na Rayon na kuzipa ubingwa wa Rwanda kwa nyakati tofauti.
Kocha Patrick Phiri alithibitisha kutimuliwa kwake simba sc na kueleza kuwa anachongoja ni stahiki zake ili aweze kurejea kwao Zambia.
1331248128Goran-Kopunovic-730835 
 "Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hilisi jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo. Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.
Phiri alisema "Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini nina kwenda nyumbani."

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top