JANA Usiku katika Mechi pekee ya Ligi Kuu England, Liverpool, wakiwa kwao Anfield, waliichapa Swansea City Bao 4-1 na kupaa hadi Nafasi ya 8 kwenye Ligi hiyo wakiwa Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4 Southampton.
Baada ya kuchezwa Nusu ya Mechi zake za Msimu, Mechi 19,, Ligi Kuu England inaongozwa na Chelsea wenye Pointi 46, wakifuata Mabingwa Watetezi Man City wenye Pointi 43, Man United 36, Suthampton na Arsenal, Pointi 33 kila mmoja.
Liverpool walitangulia kufunga kwa Bao la Alberto Moreno na kisha Adam Lallana kufanya iwe 2-0 baada Kipa Lukasz Fabianski kuokoa Mpira na kumgonga Lallana na kutinga.
Swansea walifunga Bao lao kupitia Gylfi Sigurdsson na Gemu kuwa 2-1 lakini Lallana tena akaipa Bao la 3 Liverpool na Mchezaji wa Swansea Jonjo Shelvey, ambae aliwahi kuichezea Liverpool, alijifunga mwenyewe na kuwapa Liverpool ushindi wa Bao 4-1.
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet; Can, Skrtel, Sakho; Manquillo, Henderson, Lucas, Moreno; Coutinho (Borini - 90'), Sterling Balotelli - 83'), Lallana (Markovic - 77')
Akiba: Toure, Gerrard, Lambert, Borini, Balotelli, Markovic, Ward.
Swansea: Fabianski; Richards (Rangel - 45'), Fernandez, Williams, Taylor; Britton (Ki Sung-yueng - 67'), Shelvey; Dyer, Sigurdsson, Routledge; Bony (Gomis - 62')
Akiba: Ki, Emnes, Carroll, Gomis, Rangel, Tremmel, Bartley.
Refa: Andre Marriner
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni