
Mechi hi ya utangulizi itaanza Saa 9 Dakika 45 Mchana Saa za Bongo na inazikutanisha Stoke ambayo iko Nafasi ya 11 ikiwa na Pointi 25 na Man United ambayo iko Nafasi ya 3 ikiwa na Pointi 36.
Mechi hiyo itafuatiwa na Mechi 8 zitakazoanza Saa 12 Jioni na mojawapo ni ile ya Mabingwa Watetezi Man City watakaokuwa Nyumbani Etihad kucheza na Sunderland.
Vigogo wengine ambao watacheza muda hao ni Liverpool ambao wako kwao Anfield kucheza na Leicester City wakati Arsenal, walio Nafasi ya 5, watakuwa Ugenini kucheza na Southampton, walio Nafasi ya 4, lakini Timu zote zina Pointi sawa, Pointi 33.
Siku hii ya kwanza ya Mwaka Mpya itakamilika kwa Mechi itakayoanza Saa 2 na Nusu Usiku huko Stamford Bridge wakati Vinara wa Ligi Chelsea watakapocheza Dabi ya Jiji la London dhidi ya Tottenham Hotspur.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Saa za Bongo
Alhamisi Januari 1
1545 Stoke v Man United
1800 Aston Villa v Crystal Palace
1800 Hull v Everton
1800 Liverpool v Leicester
1800 Man City v Sunderland
1800 Newcastle v Burnley
1800 QPR v Swansea
1800 Southampton v Arsenal
1800 West Ham v West Brom
2030 Tottenham v Chelsea
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni