KIKOSI cha Yanga leo jioni kimeshindwa kukamilisha
ratiba yake ya kufanya mazoezi kutokana na mvua kubwa na sasa kitaondoka kesho
asubuhi kuelekea kambini Mkoani Bagamoyo.
Kocha wa Yanga Hans
Pluijm amesema kikosi chake kilikuwa na
ratiba ya kufanya mazoezi mepesi katika Uwanja wao wa Kaunda uliopo makao
makuu ya klabu yao lakini mvua kubwa iliyonyesha leo asubuhi jijini Dar es Salaam
imeujaza maji uwanja huo.
Pluijm
amesema baada ya mabadiliko hayo sasa kikosi hicho kitaingia kambini
rasmi kesho asubuhi katika hoteli ya Kiromo ambapo ratiba ya mazoezi yao
itaendelea siku hiyo jioni.
"Tumeshindwa kufanya mazoezi leo mvua imejaza
maji pale uwanja wa klabu, nilitaka wachezaji wafanye mazoezi mepesi baada ya
mchezo wa jana lakini sasa limeshindikana,"alisema Pluijm.
"Tunaondoka kesho asubuhi kwenda kambini Bagamoyo kuanza maandalizi ya mechi zijazo tutaraji ratiba ya mazoezi yetu itaendelea hiyo kesho.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni