
Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya Tottenham na Sheffield United.
Mechi za Nusu Fainali zitachezwa kwa mikondo miwili ya Nyumbani na Ugenini kwenye Wiki inayoanzia Januari 19 na Marudiano yakiwa Wiki moja baadae.
Mapema Usiku huu wa Jumatano kabla Droo hii ya Nusu Fainali, Liverpool, wakicheza Ugenini kwa Vinara wa Timu ya Daraja la chini la Championship Bournemouth, walishinda Bao 3-1 kwa Bao 2 za Raheem Sterling na moja la Lazar Markovic wakati Wenyeji hao walipata Bao lao pekee kupitia Dan Gosling.
Kwenye Mechi nyingine ya Robo Fainali iliyochezwa pia Usiku huu huko White Hart Lane, Tottenham waliitandika Newcastle Bao 4-0 kwa Bao za Bentaleb, Chadli, Kane na Soldado.
Jumanne Usiku, kwenye Robo Fainali za awali, Chelsea na Sheffield United zilishinda Mechi zao kwa Chelsea kuichapa Derby County 4-1 na Sheffield kuifunga Southampton 1-0.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni