
WAKATI Vinara wa Ligi Kuu England Chelsea hawachezi hadi Jumatatu Usiku, Mabingwa Watetezi Manchester City wana nafasi murua kuwakamata kileleni ikiwa wataifunga Crystal Palace hapo Jumamosi.
City ndio watakaoanza Mechi za Wikiendi hii kwa kucheza Mechi ya kwanza kabisa hapo Saa 9 Dakika 45 Uwanjani kwao Etihad na Jioni Saa 12 zitafuata Mechi nyingine 6 za Ligi ikiwemo ile ya Uwanjani Villa Park ambapo Aston Villa wataikaribisha Man United ambao wako Nafasi ya 3.
Jumapili Ligi Kuu England itakuwa na Mechi mbili ambapo huko Saint James Park, Wenyeji Newcastle watacheza na Sunderland na huko Anfield ipo Mechi kali kati ya Liverpool na Arsenal.
Jumatatu Usiku ipo Mechi tu wakati Stoke City watakapoikaribisha Chelsea inayoongoza Ligi hivi sasa.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Desemba 20
1545 Man City v Crystal Palace
1800 Aston Villa v Man United
1800 Hull v Swansea
1800 QPR v West Brom
1800 Southampton v Everton
1800 Tottenham v Burnley
1800 West Ham v Leicester
Jumapili Desemba 21
1630 Newcastle v Sunderland
1900 Liverpool v Arsenal
Jumatatu Desemba 22
2300 Stoke v Chelsea
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni