
Manchester United wameibonda Liverpool Bao 3-0 Uwanjani Old Trafford na kuzoa ushindi wao wa 6 mfululizo kwenye Ligi Kuu England unaowabakisha Nafasi ya 3.
Man United walikwenda Haftaimu wakiwa Bao 2-0 mbele kwa Bao zilizofungwa na Wayne Rooney Dakika ya 12 na Juan Mata Dakika ya 40.

Kipindi cha Pili, Robin van Persie aliipa Man United Bao la 3 katika Dakika ya 71.
Ushindi huu umewafanya Man United wawe Pointi 8 nyuma ya Vinara Chelsea na Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Man City.
Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Desemba 20 Ugenini huko Villa Park dhidi ya Aston Villa.

VIKOSI:
Man United: De Gea, Valencia, Jones (McNair - 89'), Evans, Young, Carrick, Fellaini, Mata, Rooney (Falcao - 78'), van Persie, Wilson Herrera - 71')
Akiba: Falcao, Januzaj, Lindegaard, Ander Herrera, Fletcher, McNair, Blackett.
Liverpool: Brad Jones, Johnson K (Touré - 26'), Skrtel, Lovren, Moreno (Markovic - 68'), Henderson, Gerrard, Allen, Coutinho, Sterling, Lallana (Balotelli - 45')
Akiba: Toure, Lambert, Lucas, Mignolet, Can, Balotelli, Markovic.
REFA: Martin Atkinson










0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni