MGANDA
Emmanuel Okwi amewapongeza wachezaji wenzake wa Simba kwa kuonesha
ushirikiano mkubwa katika mechi ya jana ya NaniMtani Jembe 2 ambayo
Simba ilishinda 2-0 dhidi ya Yanga.
Okwi
amesema alifurahishwa na kiwango cha wachezaji wenzake na ushindi
waliopata ni zawadi tosha ya krismasi na Mwaka mpya kwa mashabiki wa
Simba.
“Mechi
ilikuwa nzuri, tumecheza kwa kujituma. Kikubwa niwapongeze sana
wachezaji wenzangu kwa kuonesha soka safi. Ushindi huu ni zawadi ya
krismas kwa mashabiki wetu”. Alisema Okwi.
Okwi alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Yanga na alitoa mchango mkubwa katika ushindi huo.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni