Coastal union ya jijini Tanga wametoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa sokoine. Katika mchezo huo wa leo uliotanguliwa na mvua na kupelekea uwanja kuwa na utelezi kila upande wametengeneza nafasi ambazo hakuna aliyeitumia vyema. Katika hatua nyingine mchezo wa ligi kuu ya vodacom kati ya mtibwa sugar na stand united ulivunjika katika dakika ya 6 sio 22 kama tulivyo ripoti hapo awali na mchezo huo unatarajiwa kuhitimishwa kesho saa mbili asubuhi.
MATOKEO MENGINE
FT | T.PRISONS | 0 | : | 0 | COASTAL UNION |
FT | JKT RUVU | 0 | : | 1 | RUVU SHOOTING |
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni