LOGO

Uongozi wa timu ya Young Africans umetoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji wake na benchi la Ufundi kabla ya kurejea tena kuanza mazoezi jumatatu ya Novemba 24 mwaka huu, kujiandaa na mzunguko wa nane wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC katikati ya mwezi Disemba mwaka huu.
Kocha mkuu wa Young Africans mbrazil Marcio Maximo alitoa mapumziko hayo kwa wachezaji wake, kufuatia baadhi ya wachezaji kuitwa na timu zao za Taifa kwa ajili ya mechi za kalenda ya FIFA na wengine kujiandaa na michuano ya Challenge Afrika Mashariki na Kati.
Wachezaji wa Young Africans walioitwa timu za Taifa ni (Tanzania), Deo Munish "Dida", Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa (Rwanda) Haruna Niyonzima, (Uganda) Hamis Kizza.
Aidha kocha Maximo pamoja na wachezaji kutoka nchini Brazil kiungo Andrey Coutinho na mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" wako nchini Brazil kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kurejea kuendelea na maandalizi ya mechi za mzunguko wa nane.
Kocha msaidizi Leonardo Neiva amebakia nchini Tanzania, ambapo kwa sasa anaandaa programu ambayo itatumika kuanzia Novemba 24, 2014 pindi kikosi kitakapoanza tena maandalizi ya kujiandaa na michezo itakayofuata.
Wachezaj wote wanatarjiwa kuripoti Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa kumalizia mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top