LOGO

ROONEY-KEPTENI-SHANGWEENGLAND itavunja desturi yake na kumkabidhi Wayne Rooney Kofia ya Dhahabu kwa kuichezea Timu ya Taifa mara 100 kabla ya Mechi ya Jumamosi Uwanjani Wembley ambapo watacheza na Slovenia kwenye Mechi ya Kundi E la EURO 2016. Mechi hiyo ya Slovenia ndio itakuwa Mechi yake ya 100 kwa Rooney kuichezea England na kawaida ni kuwa Mchezaji hupewa Tuzo hiyo ya Kofia baada ya Mechi na si kabla.
Huko nyuma, David Beckham, Steven Gerrard, Ashley Cole na Frank Lampard, wote walitunukiwa Kofia za Dhahabu baada ya Mechi zao za 100.
Hiyo Jumamosi huko Wembley, Rooney, ambae ni Nahodha wa England, ataiongoza Timu kuingia Uwanjani akiambatana na Watoto wake wawili wa Kiume, Kai na Klay.
Akiwa na Miaka 29, Rooney anaweza akaiwinda Rekodi ya Kipa wa zamani wa England, Peter Shilton, ambae aliichezea England Mechi 125 na Makamu Nahodha wa Timu hiyo, Gary Cahill, amesema Rooney anao uwezo huo.
Cahill amesema: “Rooney yuko fiti, anajitunza na anafanya mazoezi vizuri hivyo sioni kwa nini asivunje rekodi hiyo!”

ENGLAND – Wachezaji waliocheza Mechi nyingi:
1-Peter Shilton [Golikipa]Mechi 125            
2-David Beckham 115      
3-Steven Gerrard 114      
4-Bobby Moore 108
5-Ashley Cole 107 
6-Frank Lampard 106      
6-Bobby Charlton 106
8-Billy Wright 105  
9-Wayne Rooney 99        
10-Bryan Robson 90        
11-Michael Owen 89

Mbali ya Rekodi ya kucheza Mechi nyingi, pia Rooney anawinda Rekodi ya kufunga Bao nyingi kwa England na ikiwa Jumamosi atafunga Bao 1 basi atafikisha Bao 44 kwa England na kufungana na Lejendari Jimmy Greaves ambae yupo Nafasi ya 3 katika Historia ya England ya Wafungaji Bora.
Anaeshikila Rekodi ya Mfungaji Bora England ni Mkurugenzi wa Manchester United Sir Bobby Charlton mwenye Bao 49 akifuatiwa na Gary Lineker mwenye Bao 48.

ENGLAND – Wafungaji Bora:
-Sir Bobby Charlton:Goli 49 Mechi 106
-Gary Lineker:Goli 48 Mechi 80
-Jimmy Greaves:Goli 44 Mechi 57
-Wayne Rooney:Goli 43 Mechi 99

Rooney alianza kuichezea England akiwa na Miaka 17 kwenye Mechi na Australia Februari 2003 na kuweka Rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye umri mdogo kuichezea England lakini Rekodi hiyo ikaja kuvunjwa na Theo Walcott.
Lakini hadi hii Leo Rooney ndie mwenye Rekodi ya kuwa mtu alieanza Mechi ya England akiwa na umri mdogo kabisa.


0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top