LOGO

CAF-MCHEZAJI BORA 2014-LISTI YA WAGOMBEA PIA IPO!
BBC-BEST-PLAYER-AFRICA2014SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA, BBC, limetangaza Majina ya Wachezaji Watano watakaogombea Tuzo ya BBC ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2014.
Kwenye Listi hiyo yumo Mshindi wa Mwaka Jana, Yaya Toure, Mchezaji wa Ivory Coast na Klabu ya Manchester City, ambae hii ni mara ya 6 mfululizo kuteuliwa kuwa Mgombea.
Wagombea wengine wa Mwaka huu ni Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Klabu ya Borussia Dortmund, Yacine Brahimi wa Algeria na FC Porto, Vincent Enyeama wa Nigeria na Lille, Gervinho wa Ivory Coast na AS Roma.
 
Mshindi wa Tuzo hii ya BBC atapatikana kwa Kura za Mashabiki ambao wanatakiwa kuwasilisha Kura zao kabla ya Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, Jumatatu Novemba 24.
Kura zinaweza kupigwa Mtandaoni kwa kubofya hii linki: http://www.bbc.co.uk/sport/football/african/afoty-vote/2014
Pia, Washabiki wanaweza kutuma Ujumbe, wa SMS, kwenda Namba +447786202008 [Gharama atalipia Mpiga Kura].
Ukituma Ujumbe wa SMS:
-Tuma Namba 1 ukitaka kumchagua Pierre-Emerick Aubameyang
-Tuma 2 kwa Yacine Brahimi
-Tuma 3 kwa Vincent Enyeama
-Tuma 4 kwa Gervinho
-Tuma 5 kwa Yaya Toure
**Kura ni moja kwa kila Namba ya Simu.
CAF-MCHEZAJI BORA 2014:
Hivi Majuzi, CAF ilitangaza Listi ya Wagombea 25 wa Tuzo yao ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2014 na ndani yumo Yaya Toure alieitwaa Mwaka Jana na pia mara mbili mfululizo kabla ya hapo.
Washindi wa Tuzo hii huchaguliwa na Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama wa CAF.
Mshindi atatangazwa kwenye Hafla maalum hapo Januari 8 huko Lagos, Nigeria. Wagombea:
Asamoah Gyan (Ghana, Al-Ain)
Kwadwo Asamoah (Ghana, Juventus)
Dame N’doye (Senegal, Lokomotiv Moscow)
Sadio ManĂ© (Senegal, Southampton)
Emmanuel Adebayor (Togo, Tottenham)
Eric Maxim Choupo-Moting(Cameroon, Schalke 04)
Stephane Mbia (Cameroon , Sevilla)
Vincent Aboubakar (Cameroon , Porto)
Yao Kouassi Gervais (Cote d’Ivoire, AS Roma)
Wilfred Bony (Cote d’Ivoire, Swansea)
Yaya Toure (Cote d’Ivoire, Manchester City)
Fakhreddine Ben Youssef  (Tunisia, CS Sfaxien)
Ferdjani Sassi (Tunisia, CS Sfaxien)

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top