Michuano ya Cecafa Senior Chalenji sasa haipo tena baada ya waandaaji Ethiopia kujitoa, hivyo kukosa muandaaji mbadala.
Michuano hiyo ilitarajiwa kuanza Novemba 24 hadi Desemba 9, mwaka huu huko Ethiopia bingwa mtetezi akiwa ni Kenya.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka
vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Nicholas Musonye, alisema baada ya
Ethiopia kujitoa, imekuwa ngumu kupata nchi mbadala ya kuandaa michuano
kwa haraka.
“Hatukupenda, lakini imeshindikana kabisa, tulifanya kila juhudi lakini mambo yamekuwa ni magumu,” alisema Musonye.
Alisema imekuwa ngumu kupata wadhamini pia kwani waandaaji walijitoa dakika za mwisho, hali iliyowachanganya.
Michuano hiyo ilitarajiwa kuanza Novemba 24 hadi Desemba 9, mwaka huu huko Ethiopia bingwa mtetezi akiwa ni Kenya.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni