RATIBA/MATOKEO:
Saa za Bongo
Jumapili Novemba 9
Sunderland 1 Everton 1
Tottenham 1 Stoke 2
West Brom 0 Newcastle 2
Swansea 2 Arsenal 1

Arsenal walipata Bao lao Dakika ya 63 baada ya Oxlade-Chamberlain kuunasa Mpira katikati ya Uwanja na kuwachambua Wapinzani wawili kisha kumpasia Cazorla ambae haraka alimpelekea Danny Welbeck na kumhadaa Beki mmoja na kumsogezea Alexis Sanchez aliefumua Shuti lililomshinda Kipa wa zamani wa Arsenal, Lukas Fabianski.
Dakika ya 75, Swansea walisawazisha kwa Frikiki murua ya Gylfi Sigurdsson aliyopiga kutoka Mita 25 na kumshinda Kipa Szczesny.
Frikiki hiyo ilitokana na Rafu ya Gibbs kwa Barrow.

Swansea walipiga Bao la Pili Dakika ya 78 kupitia Bafetimbi Gomis ambae aliingizwa Dakika 1 tu nyuma kumbadili Wilfried Bony na kuugusa Mpira kwa mara ya kwanza tu.
Bao hilo lilitokana na kazi njema ya Jefferson Montero aliempita Calum Chambers na kutumbukiza Krosi iliyopigwa Kichwa na Bafetimbi Gomis na kutinga wavuni.
Ushindi huu umewapaisha Swansea hadi Nafasi ya 5 na kuwashusha Arsenal Nafasi ya 6.
Ligi Kuu England sasa itakuwa nje kupisha Mechi za Kimataifa na Arsenal watarejea Uwanjani Jumamosi Novemba 22 wakiwa kwao Emirates kucheza na Manchester United.
VIKOSI:
Swansea City: Fabianski; Rangel, Bartley, Williams, Taylor; Carroll, Ki; Emnes (Barrow - 67'), Sigurdsson, Montero; Bony (Gomis - 76').
Akiba: Amat, Britton, Gomis, Tiendalli, Tremmel, Fulton, Barrow.
Arsenal: Szczesny; Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs; Flamini (Wilshere - 79'), Ramsey (Walcott - 79'); Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Sanchez; Welbeck.
Akiba: Rosicky, Podolski, Wilshere, Walcott, Sanogo, Martinez, Bellerin.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni